DAY 5 : EL RACHUM
ScripturesZaburi 119:16
*Na Ev Daniely Joshuan*_
*05th September 2025*
*HATUA ZA KUUANDAA MOYO ILI KUZIPATA REHEMA ZA MUNGU KWENYE MSAMAHA*
Tuliona kwamba maandalio ya moyo ni ya mwanadamu bali jawabu la ulimi latoka kwa Bwana. Lakini tuliona pia Mungu anahitika sana namna umeandaa moyo wako zaidi ya maombi unayoomba. Watu wengi wana maisha magumu kwasababu wana mioyo mibaya.
Sasa kama umeupima moyo wako na ukaona kwamba unahitaji rehema za Mungu, pengine moyo umegeuka au haujageuka lakini umeharibika lakini unazihitaji rehema za Mungu. Kuna watu walikuwa wanatembea na Mungu vizuri na Roho Mtakatifu akawa rafiki yao. Wengine walipewa vikundi vya maombi, wengine walipewa mpaka huduma. Adui akipata nafasi kwenye moyo wako anakutenga mbali na Mungu ndipo utasikia mtu akinena maneno ya makufuru.
Sasa kama mimi nimefika mahali ambapo adui ameharibu au anataka kuharibu moyo wangu sasa nichukue hatua gani kurudiana na Mungu. Tuliona namna ambavyo Mungu aliua watoto wa Eli, tuliona juu ya Yuda, na tukaona mioyo ilivyokuwa miovu. Sasa naomba unisikilize hata kwenye kiwango hicho kuna mlango wa kutokea.
*HATUA YA KWANZA*
_*FUNGUA MSAMAHA KWA WENGINE*_
Nafikiri unajua kwamba moyo ukiwa mwovu basi chuki hazikosekani. Mchana Yesu akaniambia kama kusamehe ni ujinga basi chagua kuwa mjinga wa mwisho. Moyo ukiharibika na kuanza kumuacha Mungu, visasi, chuki, hasira havikosekani. Kuna watu wamepita mahali pagumu kwenye ndoa na ndani yao wakawa na uchungu na chuki. Sasa hatua ya kwanza ni wewe kusamehe, hauwezi kwenda kuzitafuta rehema za Mungu kwa habari ya msamaha wakati wewe haujasamehe.
Mungu wetu ni mkubwa kwasababu ya ukubwa wa rehema zake. Kuna watu wameharibu huduma kwasababu ya kushindwa kusamehe. Walionekana wakubwa madhabahuni lakini mioyo yao ni midogo haina hustamilivu. Wewe haujakuwa jitu kwasababu unajua kufundisha vizuri unakuwa jitu kwa kuweza kusamehe na kwenda mbele. Moyo ukiharibika eneo la msamaha linaharibiwa.
Hakuna mtu ataziona rehema za Mungu zitakazojifunua kwenye eneo la kumsamehe kama hajasamehe. Mungu atakusamehe sana kama utasamehe sana kama haujawahi kumsamehe yeyote haujasamehewa.
Mwingine akaniambia kusamehe kunategemeana na jambo lenyewe, maana yake haelewi kabisa, kusamehe kunategemeana na mambo yote. Nikuulize swali hapo ulipo yale unayotubu kila siku umesamehewa? Kama haujawahi kumsamehe mtu maana yake haujasamehewa. Niliwahi kukuambia kwanini usamehe.
*Mathayo 5:7*
_*Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.*_
Moyo ukiharibika hakuna anayeona makosa yake wakati mwingine unaona wengine tu. Utubaki hapo chini mpaka lini? Wako watu ambao wanaona kwamba hii alama haiwahusu lakini naomba nikuambie unaweza kuwa wewe ndiye muhanga wa kwanza na kama siyo sasa ni baadae. Kuna kiwango chako kinapimwa kwasababu ya kusamehe. Muogope sana mtu ambaye anaweza kukusamehe. Petro akamuuliza Yesu ndugu yangu anikose mara ngapi nimsamehe.
*Mathayo 18:21-22*
_*[21]Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? [22]Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.*_
Kuna watu kwenye makanisa ambao wameshindwa kusamehe kabisa. Unaweza kusamehe na Roho wa Mungu atakuambia hatua za kuzichukua kutokea hapo siyo hisia zako. Kuna mwingine ambaye utaambiwa uendelee naye na atageuka na kuwa mzuri sana.
Hakuna mtu anazifikia rehema za Mungu kama hawezi kusamehe yeye kwanza. Msamaha unamgeuza yeyote. Mungu akikusamehe unageuzwa kuwa mwenye haki, hata kama ulikuwa mbaya. Kushindwa kusamehe ndipo kunaendelea kuwafanya watu wabaya kuliko mwanzo. Kusamehe ni kumuuzia Mungu kesi.
Msamaha una nguvu ya kumgeuza yeyote.
*Mathayo 6:14*
_*Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.*_
Wako watu ambao wanahitaji msamaha wa Mungu hakuna namna ambavyo utaona msamaha wa Mungu kama haujasamehe wengine. Njia ya kwanza ya wewe kuziendea rehema za Mungu ni wewe kusamehe kwanza kabla ya wewe kusamehewa. Hii njia ya kwanza ya kuandaa moyo ili Mungu akusamehe. Samehe wengine na yeye atakusamehe. Unataka Mungu akusamehe fungua malango wa msamaha kwa moyo wako wote.
Katika kiwango cha juu cha hasira yako ni hekima kwako kusamehe. Katika kiwango cha hasira yako samehe. Moyo ukiharibiwa watu wanajaa moyoni. Moyo ukianza kuharibika unaanza kubeba mabaya moyoni.
*HATUA YA PILI*
_*KUANZA UPYA KURUDISHA AMRI ZA MUNGU MOYONI MWAKO*_
Nafikiri unatakiwa kujua kwamba moyo ukiharibika zile amri za Mungu zinakuwa kitu kidogo kwako. Neno usiibe linakuwa rahisi kwako, neno usizini linakuwa jepesi kwako. Unapaswa kuanza kurudisha amri za Mungu katika moyo wako. Unaanza kutafakari kwa upya amri za Mungu.
Mungu anapoona unaanza kurejesha moyoni mwako amri zake anaanza kuachilia rehema zake. Hii ni hatua ya pili ya muhimu sana. Rehema zozote unazomuomba Mungu wakati umekataa kurudisha amri zake ni batili. Nafikiri unajua Neno kupakia (Restore) ni zaidi ya kurudisha. Unapoanza kupakia upya utafikia rehema zake.
Zamani watu walikuwa wanafundishwa amri kumi za Mungu wakiwa shule ya jumapili ili kukaa ndani ya mioyo yao. Sikuhizi si jambo la kutisha ukikuta mtu mwizi ndani ya kanisa kwasababu hajaweka amri za Mungu moyoni mwake. Amri za Mungu zinaweza kuwa kichwani kwako lakini si ndani ya moyo wako.
*Zaburi 119:5*
_*Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.*_
Huyu ni Daudi katika matengenezo yake anaanza kupakua upya amri za Mungu.
*Zaburi 119:12*
_*Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.*_
Anarudia maneno haya kwasababu anapakia amri za Mungu ndani yake. Ndiyo maana anasema atakapokuja roho wa uzima ataandika sheria zake mioyoni mwetu. Mungu hataki uzikariri amri zake anataka zikae moyoni mwako. Zikikaa moyoni mwako ukivunja utaumia ndani ya moyo wako.
*Zaburi 119:16*
_*Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.*_
Huyu ni mtu wa kimatengenezo lakini anachokifanya ni kupakua kiroho.
*Zaburi 119:23*
_*Wakuu nao waliketi wakaninena, Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.*_
Rehema na msamaha wa Mungu ambazo unazitakufuta bila hatua hizi ni kukimbiza upepo. Daudi alijua kuna hatua za muhimu za kurejesha amri za Mungu kwenye maisha yake. Somo ili limekuja ili uende ukaweke kwa upya amri za Mungu moyoni mwako.
*Zaburi 119:26*
_*Nalizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako.*_
Upakuaji wa kiroho wa amri za Mungu moyoni mwako. Unapofanya namna hiyo unazisogelea rehema za Mungu.
*Zaburi 119:33*
_*Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hata mwisho.*_
Umebeba nini moyoni mwako? Naomba nikukumbushe kuna mari Mungu ameziweka. Unaweza kusema hatuko chini ya sheria ni kweli lakini tuko chini ya sheria wa Roho wa uzima na amri zake ameandika moyoni mwetu. Ukifuata hizi kanuni utaona rehema za Mungu.
*Zaburi 119:64*
_*BWANA, dunia imejaa fadhili zako, Unifundishe amri zako.*_
Daudi anasema ninajua kuna rehema zako lakini lazima aamue kupakia kwa uoya amri zake ndani ya moyo wako. Si kupakia kichwani bali moyoni mwako.
*Zaburi 119:68*
_*Wewe U mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako.*_
Sijui kama hii inakusaidia na kama leo haikusaidia kuna wakati utakutana na mtu ambaye atakuambi nimeharibu na sijui nategenezaje na Mungu sasa ukisema hautakuwA NA KITU CHA KUMWAMBIA afadhali usingesoma maneno haya.
Naomba nikuambie neno moja gumu jehanamu kule watu wamekariri amri zote kumi na wanazisema kutoka moyoni lakini wamechelewa. Ayubu alinyenyekeshwa akapata kujifunza amri za Mungu. Ayubu alijisemehea kwamba yamkini watoto wangu wametenda dhambi maana yake alijiondoa. Meseji kwenye kitabu cha Ayubu ni kwamba Mungu anaweza kumyenyekesha yeyote.
Ilikuwa vyema kuteswa ili ujifunze amri za Bwana. Ungewezaje kuwa ulivyo kama si yake yaliyokukuta ilikuwa vyema kupata hayo mateso.
*Zaburi 119:80*
_*Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, Nisije mimi nikaaibika.*_
*Zaburi 119:112*
_*Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako, Daima, naam, hata milele.*_
Nataka utafakari hizi amri za Mungu usiku wa manene ndiyo maana nakuinyesha mistari hii.
*Zaburi 119:124*
_*Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe.*_
Umeona uhusiano kati ya kuingiza amri za Mungu moyoni na uhusiano wake na rehema zake. Kama ambavyo ukisamehe na wewe unarehemiwa ndivyo ilivyo kwenye kuweka amri za Mungu moyoni mwako.
*Zaburi 119:145*
_*Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike; Nitazishika amri zako.*_
Hii Zaburi ya 119 ni ya mwqnaune ambaye alikaa chini akaamua kuzitafuta rehema za Mungu na moja ya ufunguo ambao alikumbuka ni ufunguo wa kuzalisha upya amri za Mungu ndani ya moyk wake.
*Zaburi 119:155*
_*Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako.*_
Hakuna namna ya kuzifikia rehema za Mungu mpaka utakapopakua amri za Mungu moyoni mwako. Hapa anaongea na watu ambao wako ndani ya kanisa wanajua kuhusu sheria za Mungu na wamekosea au wanaishi kwenye makosa. Hili uweze kuzipata rehema za Mungu nenda na pakua amri kumi tena na kuhifadhi ndani ya moyo wako.
*Restoration Gospel Commission Ministry,*
*P.O.Box 32520,*
*Goba Centre, Dar es salaam, Tanzania,*
*Email: info@rgcm.org,*
*Contact: +255 764 711 544,*
*Web: https://www.rgcm.org.*