Shule ya Bibilia

“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”
— Zaburi 119:11

Karibuni katika Shule ya Biblia – na Evangelist David Joshua (RGCM).
Hapa tunakualika ujiunge nasi katika kumtafuta Bwana kwa maarifa na NENO LA MUNGU,kuanzia kunywa maziwa hadi kufikia kula MEGO KAVU - Chakula Kigumu cha watu wazima.

Unahitaji Maombi na Ushauri?

Wasiliana nasi moja kwa moja:

📞 +255-715-402-238
📞 +255-762-738-462

Pia unaweza kutuma maoni au maombi yako nasi tutaomba nawe kwenye namba hizo.
“Kula na Ukue Kiroho...” — Luka 8:5-14

Omba Sasa Soma Biblia

Habari Njema ya Bwana Yesu Kristo

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; — Tito 2:11 —

Haleluya! Bwana Yesu asifiwe sana rafiki zangu. Yesu anakupenda sana na anatamani umgeukie na kumwamini yeye kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Neema hiyo iliyofunuliwa ni Yesu Kristo, naye yu karibu kurudi, ndugu yangu. Hebu chunguza maisha yako: akisema sasa anarudi, je, utaketi naye mawinguni?

Ndugu, jehanamu ipo na mbingu ipo. Neno la Mungu linasema katika Matendo ya Mitume 3:19: “Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.” Siku ya mwisho ipo na inatisha. Ndugu yangu, badilisha tabia yako na mwenendo wako kabla hazijaja siku za hatari. Maana kumbuka kiburi cha mwanadamu kina mwisho.

Ikiwa umemwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, fuatisha sala hii:

"Ee Bwana Yesu, nakiri dhambi zangu na makosa yangu yote niliyokukosea. Leo nimeamua kukupokea kuwa Bwana, Mwokozi, na Kiongozi wa maisha yangu. Ingia ndani ya maisha yangu, fanya makao yako. Amina."

Tupigie namba hizi au tuma ujumbe wa SMS/WhatsApp:
0715-402-238 au 0762-738-462
ili tuweze kuomba nawe pia.

Mahubiri na mafundisho yenye kubadilisha

Mtd 2:42

Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Shuhuda zenye kubadilisha maisha

Ufunuo 12:11

"Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa"

Tovuti Yetu

Tunaeneza Injili kupitia mafundisho, maombi na mahubiri katika jina la YESU KRISTO.

“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”
— Wafilipi 4:6

Mungu akubariki sana unapotafuta uso Wake! 🙏