cover

DAY 1 : EL RACHUM

Ev Daniel • RGCM-BOKO • Apostolic Church • 2025-09-03
ScripturesZaburi 79:8

*Na Ev Daniely Joshuan*_ *01 September 2025* Mungu hana sifa nyingi lakini moja ya sifa aliyonayo ni Mungu wa rehema. * Wote tunataka rehema za Mungu. Haijalishi wewe ni mwenye dhambi au mwenye haki. Sisi sote tunazihitaji rehema za Mungu na tunahitaji viwango vya kina sana kuzifikia rehema za Mungu. *Zaburi 79:8* _*Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu, Rehema zako zije kutulaki hima, Kwa maana tumedhilika sana.*_ Rehema za Mungu zinaweza kuwafunika watu. Hakuna mwanadamu anayeishi ambaye hajqfunikwa na rehema za Mungu. Hakuna namna mwanadamu anaweza kuishi bila kufunikwa na rehema za Mungu. Hakuna namna ambavyo Mungu anaweza kushirikiana na Mwanadamu pasipokuwa na rehema zake. Hapo ndipo linakuja swala la ubinadamu mahali ambapo mtu ni mtu na Mungu anabaki kuwa Mungu. Mungu aliwatenga wana wa Israeli awe mfalme wao. Mungu alitaka kuwatawala mpaka na leo lakini walipoona kuna watu wanatawaliwa na wafalme basi wana wa Israeli wakataka mfalme. Israeli walivutiwa na wafalme wa dunia namna wanavyotawala. Nataka kukuambia ni hatari sana mwana wa Mungu kutamani kuishi kama watu wa dunia hii. Mungu anaweza kumsamehe mtu aliyetenda uovu lakini hawezi kumsamehe mtu ambaye moyo wake ni mwovu. Sauli hakutenda tu maovu bali moyo wake ulikuwa mwovu. Daudi alikuwa mtu wa moyo wa Mungu lakini alitenda makosa. *Mathayo 15:22* _*Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.*_ Unajuaje kwamba umefika mahali pa kuwa na moyo mwovu ni mahali ambapo hauna hukumu ya ndani. Moyo wako unakuwa tayari umegeuka. Moyo wa mwanadamu unageuka na anakuwa mtu mwingine. Mwanadamu akiharibiwa na shetani hafanani na shetani anakuwa mbaya kuliko shetani. Rehema za Mungu zi juu kazi zake zote. *Isaya 54:7* _*Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.*_ Kuna kiwango cha neema ambacho anakukusanya. Anakusanaya waliotawanywa. *Maombolezo 3:22* _*Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.*_ Ukijioeleka mbele za Mungu kwa rehema maana yake iko juu ya uhamuzi wake. Ni muhimu sana kujua kwamba kuna kutembea na Mungu kwa imani hapo unaamini kila kitu kinawezekana lakini kuna kutembea na Mungu kwa maarifa, hapo unamtambua Mungu unayetembea naye hauwezi kushindwa, hauwezi kukata tamaa hauwezi kurudi nyuma utaendelea kusonga mbele kwasababu unamjua Mungu wako. Hata katikati ya shida hautaogopa. Akikuelekeza jangwani unajua kwamba anakuwazia mema. Nitakuinyesha kiwango kimoja cha rehema za Mungu na nitakuinyesha ni rehema za Mungu wana wa Israeli kupita jangwani. *Kutoka 13:17-18* _*[17]Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri; [18]lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.*_ Israeli waliona wanateseka jangwani lakini ilikuwa ni safari ya rehema. Kwasabbau hawakuwa na maarifa hata ile rehema haikuwasaidia. Wangepita njia ya wafilisti wangefika haraka. Kuna mambo mengine ni magumu unapitia lakini ni rehema za Mungu. Rehema za Mungu si kukupa tu unachotaka. Daudi alichagua kuangukia kwenye mikono ya Mungu kwasababu kwa Mungu kuna rehema lakini si kwa wanadamu. Ni heri uanguke kwenye mkono wa Mungu maana atakurehemu. Kuna namna ambavyo unaziita rehema za Mungu atakusamehe na kukurejesha iwe ni kwenye kipawa chako au huduma yako. Ndani ya siku hizi ukinisikiliza kwa makini utamuona Mungu wa rehema kwenye maisha yako. Watu ambao waliotapikwa watarejeshwa tena na kupata rehema. Waisraeli walikaa jangwani miaka 40 lakini viatu vyao havikuchakaa wala nguo zao hicho ni kiwango cha namna gani cha rehema. Wangekubali kufundishwa na rehema za Mungu wangekuwa mbali sana. *Danieli 2:18* _*ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli.*_ Nitakuonyesha kiwangu kingine cha rehema cha kuingilia kati. Kina Daniel wanaambiwa kuna ndoto imeotwa na waganga na wachawi walishindwa kutafsiri wakina Danieli wanaenda kuomba rehema ndani ya siku tatu Mungu anawafunulia ndoto na maana yake. *Hosea 2:23* _*Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.*_ Mungu yuko tayari kuwaonyesha rehema wasio na rehema, yuko tayari kuachilia msamaha. Tutajifunza namna ya kuomba rehema kwa namna zote. Tutaangalia namna ya kuitia rehema za Mungu ili kufungua malango wa kuingilia kati kwenye huduma, kazi,ofisi n.k. Ni kusudi la Mungu kwa siku hizj thelathini kwamba yeyote anayehisi kushindwa, kukataliwa Mungu atamrejesha karibu. *Zaburi 23:6* _*Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.*_ Huu ni ufungui wa rehema, hakuna mwanadamu anayeishi pasipo kushikamana na rehema za Mungu. Wema na fadhili za Bwana zitanifuata siku zote za maisha yangu. Nataka ili andiko liko hai kwenye maisha yako na si kwasababu unasoma, kuna vitu si vya kusoma haviwi vyakwako kwasabahu umevisoma n8 kwasababu umevielewa. Rehema za Mungu lazima zikufunike kila unapokwenda. Waamininwanahitaji rehema za Mungu kuliko mtu yeyote. Kuna kiwango cha rehema za Mungu ambazo Daudi alikuwa anatembea nazo. Unapofika kwenye andiko ili ni kiwango kikubwa mno. Andiko linakuwa hai kwako kwasababu ya maarifa na Imani. Anaposema hakika maana yake ni kiapo. Mungu anshudiana na sisi mmoja mmoja kulingsna na rehema zake, hakuna ujumla jumla. Sijui wewe na Mungu kwenye upande huu mna nini lakini ni mmoja mmoja. Na nataka ulie kwa nirehemu mwana wa Daudi. Nataka uziite rehema za Mungu kwako na wikii hii nzima ni rehema za Mungu kwako na wiki inayofuata nitakuinyesha namna ya kuita rehema za Mungu kwa kiwango cha hekima. Wiki inayofuata nitakuinhesha namna ya kuzitafuta rehema za Mungu kuingilia kati mambo. Kuna mambo umeamka kuvunja yalikuwa si ya kuvunjwa yalikuwa ni ya kuita rehema za Mungu. Kuna mambo ulitaka asema lakini hayakuwa ya yeye kusema.

Comments

No comments yet.

Please login to comment.