Kuinua Jeshi la maombi
ScripturesMathayo 26:41
Kuinua Jeshi la maombi
Mathayo 26:41. Kesheni mwombe,msije mkaingia majaribuni
Vitu 3 vimetajwa kwenye huu mstari
1. Kukesha
2.Kuomba
3.Majaribu
Kukesha si kutokulala Bali kuwa makini.It is all about spiritual sensitivity.Dunia ilivyo Sasa kama hatuombi na hatutilii mkazo maombi, tuko hatarini kwani mikwamo mingi na shida nyingi zinazotupata ni za kiroho
1. Mkristo halisi na makini ni yule anayeomba.Mkristo dhaifu ni yule asiyeomba.Ndoto na maono hudhihirisha Kinga za kiroho tulizonazo.Shetani haogopi kelele lakini anaogopa Nini kimebebwa kwenye kelele.
2. Maombi ni kujidhabihu(sacrifice)
3. Maombi ni silaha kuu( a great weapon)
4.Maombi ni uwezesho wa kukua kiroho au badiliko.Maombi lazima iwe ni tabia yetu.Kuna tabia mbaya zinaweza kuondoka tukiomba.
Kwa Nini Jeshi ?
1.Hakuna jeshi la mtu mmoja, jeshi ni timu. Mathayo 18:19
2.Jeshi Lina nidhamu ya Hali ya juu na Ndivyo ilivyo maombi yanahitaji nidhamu ya Hali ya juu .Yesu alieleza haya ktk Mathayo 5:6:7
3.Jeshi ni mafunzo na maombi ni fundisho na wanafunzi walimwambia Yesu utufundishe Kusali Mathayo 6:9-13 Luka 11:1-4.Tukumbuke mwombaji namba Moja ni Roho Mtakatifu.
4. Maombi ni kujidhabihu ni sacrifice.Kama walivyo wanajeshi Huwa tayari Kwa chochote na wakati wowote.Mwombaji hakati tamaa,amejitoa Mhanga Luka 18:1 Imewapasa kumwomba Mungu siku zote bila kukata tamaa.
5.Nchi zote Zina majeshi ya wakati wa Sasa na ujao.Maombi pia ni mpango wa Sasa na wakati ujao.Jeshi linahakikisha usalama wa nchi Sasa na baadaye.Maombi huhakikosha usalama wa kanisa la Mungu Sasa na baadaye.Tukumbuke si Kila tunapopiga magoti tunaomba Msamaha.Magoti mengine ni ushindi Mwanza 49:1
6.Maonbi ni mamlaka na Jeshi pia ni mamlaka( Authority).Tukiomba tunaamrisha vitu vifanyike.
Namna ya kushinda kupitia Maombi
1.Jeshi hushindana na kushinda Ndivyo Kwa jeshi la waombaji,hushindana na kushinda. Yeremia1:4-10
2.Jeshi la maombi lazima lijifunze kutumia silaha ya maombi 2Wafalme6:1-20
3.Jeshi la maombi hupeleleza Kwa maombi.Tunaweza kutumia maombi kupeleleza na kupata Siri ktk ulimwengu wa roho.
4.Jeshi la maombi ni ulinzi.Linaweza kulinda,madhabahu, Watumishi wa Mungu, kazi,biashara,masomo,ndoa ,Watoto,mashamba,nyumba, nk
5.Jeshi la maombi Liko tayari kuteka 2Wakorintho 10:3-5